Rhumba ya Jirani.

Lemme tell y'all something I discovered,
fixing shit unlocks a good feeling in you.
A little backstory, niko kejani nimechill napanga venye siku ya kesho itakuwa. It's around 9/10 pm hapo, niko ndani ya duvet, hii baridi ni mbaya, but I'm kind of happy one ni ju Manchester imenyoroshwa, na Kenya imeweza kuingia quarter finals za Chan.
Niko easy, scrolling through, checking emails, sending CVs, na proposals hapa na pale, yenye itanasa ya kwanza. Hii story ya kutafuta shillingi, eeeei inatumaliza! Nimejiambia, wacha ni scroll simu kidogo, kabla usingizi ikuje, nilale kidogo, before usingizi ipotee hapo saa name, tisa, ju ya mawazo ya venye maisha yangu imestagnate, inakuja kukuja. Kiasi kiasi, nastukia niko kwa giza!
Niko zile za Kplc hao, wameanua stima. Naamua nitoke kwa bed, niende ni connect simu kwa charger, ndio ile time stima itarudi, nitaamka asubuhi nipate simu ikiwa full charge. Nikiplug simu hivi, naona, charging. Nikajijazia kumbe ni bulb imeungua. Kuchungulia Mpesa, naona inachezea titration figures, nikajiambia kesho nikiwahi pahali, nipate dooh, nitapitia kwa shop nikikuja na bulb ingine.
After nimeset alarm ya kuamka kesho ngware, na nikaplug simu ina charge, mimi huyo, kwa duvet. Next morning, naamka, kushower, kubahatisha ka utapata shillingi. Kwa bahati mzuri, I get something to earn me some coins hapa na pale for a few days, nilibuy bulb on day one, but design naingia kejani nikiwa nimebeat, naingia kejani kama nimekula, naoga, then nalala, hadi nguvu ya kuscroll simu hakuna.
Hii kazi ya freelancing, kuna siku zinafika hauna kazi kabsaa! After a busy few days, nikaukiwa pande yangu, nikakumbuka hayaa, nafaa kuchange bulb. Kutoa bulb yenye ilikuwa nikaweka yenye nilikuwa nimebuy, kuweka on, hayaa! Pia hio haiwaki. Nikajiuliza sasa hii ni mambo gani. Sasa ni kuanza kupiga hesabu ya pesa ya kuita fundi, na ya bulb holder yenye sikuwa nimepangia.
Leo nimesema, wacha niangalie hii maneno nini mbaya nayo, ndio hata fundi akikuja asione nikikuwa green asiniitishe pesa itafanya ni faint niende niongezwe maji Kenyatta.
Mimi huyo nimezima main switch, mimi hapana taka mchezo na stima. So nimechukua stool nikapanda niangalie nini mbaya na hii bulb holder.
Kutoa bulb hivi, one of the screws ina anguka, turns out, ni one of the screws huko ndani ilikuwa loose. Nikasema wacha nitoke nipige lap, nitafute pahali naweza pata star shaped screwdriver, niulizie ni pesa ngapi ninunue, nikuje nayo nione kama naweza rudisha hio screw.
Comments
Post a Comment
Is a pleasure to keep you as my reader entertained. Peace✌️