Miss Anonymous 2
Continued from here-->> Miss Anonymous Ju ya kuwa street smart kiasi tu, niliweza kutoka kuwa mgeni wa serikali bila kesi kuwa ngori. Vile natoka though, weeeh! Nanuka, niko mchafu, usingizi, kitu nataka ni kufika tu kejani nioge, nipite kwa mathe nikule, nilale. Nafika hivi ploti, watoto wa jirani wakinicheki wanahepa tu wakilia, kwani nakaa mnyama nini? Wamama wa ploti, najua wameshapata story mpya na mimi, but haidhuru, watabonga kisha watalala. Venye nimeshiba, napiga shower nitoe stench na misuli inyooke kidogo kisha nalala. Nastukia mlango inabishwa, kuangalia saa ni saa kumi na moja jioni. Weeh, nimelala kama maiti za pale Chiromo.😅 Kumbe ni arif yangu Timo, na venye nilikuwa nimejitayarisha na maneno nikidhani ni landlord. 😅😅 Namfungulia mlango aingie, but anaingia akiniuliza nimepotelea wapi, ati amekuwa akinitafuta siku kadhaa. Nikienda kuona venye nitamjibu, ghafla bin vuu, simu inalia. Kuenda kucheki ni nani anapiga, nastukia ni ule Miss Anonymous...